Swahili year 10

Created
Pages

SWAHILI YEAR 10 END OF SEMESTER EXAMS SOMA MAKALA HAYA KISHA UJIBU MASWALI Siti amelelewa karibu na bahari huko Zanzibar. Alizoea kucheza ndani ya maji na kaka yake, lakini, tofauti na kaka yake, yeye kamwe hakujifunza kuogelea. Kaka yake alipokuwa akijifunza kuogelea, Siti alijishughulisha na mambo mengine. Anasema “sisi tunaishi kwenye kijiji cha wavuvi, hivyo maji ni maisha yetu. Kila siku, watu hutumia majahazi kusafiri na kuenda kwenye visiwa vilivyo jirani; ni wachache wanaotumia meli kwani ni ghali”. Kwa hiyo, mwaka uliopita, alipokuwa na miaka 24 aliamua kujifunza kuogelea. Alijiunga na kundi la marafiki wanawake na wakafundishwa kuogelea. Mwalimu wao alikuwa ni gwiji wa kuogelea kutoka visiwani Zanzibar. Ilimchukua madarasa 15 kuweza kuogelea. Alijifunza kuelea, kuogelea na kuokoa wengine kwa kutumia vijiti na madebe. Alifanya mazoezi mengi kila wiki na sasa anaweza kuogelea vizuri sana kwa zaidi ya mita 200. Tangu kuwa mwogeleaji mzuri sana ameamua kuwa mwalimu wa kuogelea na kuwafundisha ujuzi huu wasichana wengine kijijini kwake. Anaamini kwamba kila mvulana na kila msichana anastahili kuweza kuogelea.

Worksheet Image