KISWAHILI YEAR 4

Created
    English
  1. Other
  2. 4 Grade
  3. Rose Reuel
Best for asynchronous learning and homeworkAssign in student-paced mode
Best for live in-class or video conferencing lessonsStart teacher-led lesson
Preview as student
Worksheet Image

KISWAHILI YEAR 4. 1. Andika Insha kuhusu ‘ Mnyama nimpendaye ‘. ( alama 10) 2. Andika wingi wa maneno . (alama 4).  Sahani  Msichana  Gari  Mdudu 3. (a). Andika majina ya rangi hizi : ( alama 4 ).

Worksheet Image

(b). Taja rangi zozote nne zinazopatikana kwenye Upinde wa mvua. ( alama 4 ). - - - - 4. Unda maneno ukitumia sauti zifuatazo: ( alama 3 ). (a). -pa (b). -e ©. -shu Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali. ( alama 15).

Worksheet Image

PAKA NA PANYA Hapo zamani za kale , paliishi wanyama wawili walioitwa Paka na Panya. Walikuwa wanapendana sana. Panya waliishi kwa babu yao mkuu. Walikuwa wanapewa chakula cha aina tofauti hadi wakanona hadi nguruwe. Walikuwa wanacheza kwa furaha kutokana na shibe. Siku moja, Paka mmoja mkubwa aliwatamani Panya sana kwa vile walikuwa wanono. Aliamua ya kuwa hata kama walikuwa na urafiki mkubwa na Panya, atakuwa akiwala mmoja mmoja. Paka alianza kazi yake katika nyumba ya Panya na kila siku alikuwa anaua mmoja na kumla. Panya waliookoka walikuwa na huzuni na pia hofu kubwa. Paka aliyekuwa amekonda kama ng’onda kwa sababu ya kukosa chakula, sasa alikuwa amenona kama nguruwe kwa sababu ya kuwala Panya. Panya waliendelea na kupungua zaidi na kutokana na kupungua huko. Walifanya mkutano wa kuzungumzia unyama wanaofanyiwa na Paka. Pia, hatua ambayo wangemchukulia Paka. Panya walikubaliana ya kuwa watamfunga Paka kengele shingoni ili akija, wawe wanamsikia. Panya waliulizana ni nani angemfunga Paka kengele shingoni. Panya wote walinysmaza kutokana na uoga. Panya mmoja alijitolea kumfunga Paka kengele shingoni. Panya wengine walifurahia kusikia haya. Panya huyo alipomwona Paka,alimrukia kutaka kumfunga lakini Paka alimshambulia Panya kwa hasira na njaa aliyokuwa nayo. Panya huyo aliuliwa na akaliwa. Paka aliendelea kunona zaidi kutokana na kufanikiwa kuwauwa Panya. Panya walipoona ya kuwa wangeisha, waliamua watoroke na wakahamia msituni. Kyle walikotorokea, hakuwa na Paka hata mmoja. Panya walifurahia sana kwa sababu walijua ya kuwa wangeendelea kuongezeka na kuishi maisha mazuri yasiyokuwa na usumbufu. Maswali 1. Paka walikuwa wanaishi wapi?(alama 2). 2. Paka alikuwa anawatendea Panya unyama gani? (alama 2). 3. Panya waliamua kumfanya nini Paka ndio awache kuwala? (alama 2) 4. Ni nini kilimtendekea yule Panya aliyejitolea kumfunga Paka kengele shingoni? (alama 2). 5. Panya walihamia wapi? (alama 1). 6. Maisha ya Panya yalikuwa vipi walikohamia? ( alama 2).

Worksheet Image

7. Je, unafikiri Panya na Panya wanaweza kuwa marafiki tena leo? { ndio au la }? ( alama 1.) 8. Kwa nini Paka aliyeonekana kukondeana sasa kanona kama nguruwe ? ( alama 2 ).